Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana ni viongozi wa leo na si kesho; Asema Ban

@United Nations

Vijana ni viongozi wa leo na si kesho; Asema Ban

Kongamano la siku mbili la vijana limeanza leo mjini New York, Marekani, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Lengo la kongamano hilo ni kushirikisha vijana katika maandalizi ya ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015, na kuhakikisha sauti ya vijana hao inasikika katika mambo ya kisiasa na kiuchumi ya nchi zao.

Rais wa ECOSOC, Martin Sajdik, amesema, asilimia 25 ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana, lakini asilimia 43 ya vijana bado hawana kazi, na kwamba hali hii inapaswa kubadilishwa!

Wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo, mtengenezaji wa filamu Lisa Russell, ameandaa shairi lililokaririwa na vijana kutoka Marekani wakisema... (sauti ya vijana)

Wamesema, dunia tunayoitaka ni dunia inayotukubalia, na huyu kijana mweusi wa miaka 20 amejitambulisha akisema anahangahika kama kijana wa mitaani Nairobi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipohutubia ukumbi, amesema:

“Kawaida watu wanasema kwamba vijana ni viongozi wa kesho, lakini maoni yangu ni tofauti, naamini kwamba vijana ni viongozi wa leo tayari. Nusu ya watu duniani wako na umri chini ya miaka 25, kwa hiyo tunahitaji juhudi za vijana hao sana. Vijana, ajenda ya maendeleo baada ya 2015 ni hatma yenu, kwa hiyo inabidii iwe ajenda yenu”

Halikadhalika, Rasi wa Baraza Kuu, John Ashe, naye akazungumza… “Sisi tunachukua maamuzi kuhusu hatma yenu, lakini hamjashirikishwa. Hivi najibu maswali ya hawa vijana: Lazima mjihusishe! Msipofanya hivo, na baadaye ajenda itokezee ambayo haitawaridhisha, hamtaweza kulaumu mtu mwingine isipokuwa nyie. Kwa hiyo ujumbe wangu ni huo: mjihusishe! “