Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mauaji ya raia Ghazni

UNAMA yalaani mauaji ya raia Ghazni

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Afghanistan, UNAMA umelaani vikali mauaji ya raia 12 kwenye jimbo la Ghazni nchini humo.

Taarifa ya UNAMA imesema mauaji hayo yalitokea baada ya magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara kuelekea kwenye harusi kulipuliwa na vilipukaji vilivyokuwa vimetegwa barabarani na kusababisha vifo vya wanawake Sita, watoto wanne na madereva wawili wa magari hayo.

Naibu Mkuu wa UNAMA Nicholas Haysom amekaririwa akisema kuwa kitendo cha matumizi ya vilipukaji vya kutengeneza vimezidi kuleta majanga Afghanistan ambapo kuanzia mwezi Januari raia zaidi ya 300 wameuawa ilhali 695 wamejeruhiwa kutokana na matumizi ya vilipuzi hivyo.

Bwana Haysom amesema hilo linasikitisha na amesisitiza wito wa UNAMA wa kutaka vikundi vyote vinavyopinga serikali Afghanistan kusitisha matumizi ya silaha hizo kwani zina madhara makubwa kwa raia.

Amesema matumizi yake yanaweza kuwa kitendo cha uhalifu wa kivita na ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za haki za kimataifa za kibinadamu ambazo kila upande zinawajibika kuzingatia.

UNAMA imetuma rambirambi kwa familia za wafiwa.