Malalamiko yoyote dhidi ya matokeo ya uchaguzi Malawi yazingatie kanuni:Ban

31 Mei 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema amekuwa akifuatilia kwa makini mchakato wa uchaguzi nchini Malawi ikiwemo kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Ijumaa ya tarehe 30 mwezi huu kulikofanywa na Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.

Ban amekaririwa katika taarifa akisema kuwa kwenye kipindi hiki muhimu kwa Malawi, vyama vyote vya siasa viendelee kusihi utulivu miongoni mwa wafuasi wao na wajizuie kwa kuzingatia azimio la amani la Lilongwe la tarehe 10 mwezi Mei.

Ametaka pande zote kuheshimu vifungu vya katiba huku akirejelea wito wake wa awali kwa wagombe kufuata kanuni za kisheria iwapo kuna malalamiko yoyote.

Katibu Mkuu ametaka viongozi wa kisiasa kuwasihi wafuasi wao kushirikiana ili kuimarisha demokrasia na kujenga utulivu nchini Malawi.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter