Tuna wasiwasi kuhusu kesi dhidi ya mtetezi wa haki za binadamu Burundi:UM

30 Mei 2014

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Umoja wa Mataifa umesema kuwa una wasiwasi mkubwa juu ya mustakhbali wa mtetezi wa haki za binadamu nchini Burundi Pierre Claver Mbonimpa.

Mbonimpa kwa sasa anashikiliwa kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa kutokana na maoni aliyotoa kupitia kituo kimoja cha radio nchini Burundi.

Msemaji wa Umoja huo Stephen Dujarric amewaambia waandishi wa habari kuwa hawana taarifa za kuthibitisha madai yaliyotolewa na Mbonimpa lakini …

“Tunasihi mamlaka zote nchini Burundi kuzingatia haki kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya haki za binadamu ambavyo Burundi imejikita kuzingatia, na tutaendelea kufuatilia mchakato wa kisiasa Burundi.”

Halikadhalika Dujarric amesema wana hofu kubwa kutokana na vikwazo vya haki za kiraia dhidi wafuasi wa vyama vya siasa, vyombo vya habari na mashirika yasiyo ya kiraia hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter