Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa ujumbe wa UM Sudan Kusini kufikia ukomo wa jukumu lake Julai:

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM Sudan Kusini na mkuu wa UNMISS Hilde Johnson. (Picha:UN /Tim McKulka)

Mkuu wa ujumbe wa UM Sudan Kusini kufikia ukomo wa jukumu lake Julai:

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, Hilde Johnson ametangaza kuwa atafikia ukomo wa jukumu lake Julai mwaka huu.

Bi. Johnson ametangaza hayo alipokutana na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais Salva Kiir kuhusu mamlaka mpya ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS iliyoidhinishwa wiki hii na Baraza la Usalama.

(Sauti ya Bi. Johnson)

Nimetumia pia fursa hiyo kujadiliana na Rais kuhusu majukumu mapya. Ni tofauti na yale ya awali nilipokuja kama mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu mwaka 2011. Na hii itaamanisha mabadiliko ya ujumbe wa sasa. Na hivyo nimemjulisha Rais kuwa ifikapo Julai siku ya Uhuru ningalikuwa nimekamilisha miaka yangu mitatu ya uwakilishi maalum ambayo si kawaida kwa wadhifa huio kwenye ujumbe wa ulinzi wa amani na hususan kwenye mzozo wa aina hii. Kwa hiyo nimemjulisha Rais kuwa nimefikia mwisho wa awamu yangu na nitaondoka Sudan Kusini.”

Bi. Johnson amesema ilikuwa ni heshima kubwa kwa yeye kuhudumu Sudan Kusini na ataendelea kuwepo kwa wiki kadhaa.