Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio dhidi ya kanisa CAR, idadi ya vifo yaongezeka, 27 hawajulikani waliko:UNHCR

Watoto katika moja ya kambi za muda za wakimbizi wa ndani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Picha:UN/Evan Schneider))

Shambulio dhidi ya kanisa CAR, idadi ya vifo yaongezeka, 27 hawajulikani waliko:UNHCR

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Huko Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR, idadi ya waliouawa katika shambulio dhidi ya kanisa siku ya Jumatano imefikia 17 ilhali wakimbizi wa ndani 27 hawajulikani waliko. Taarifa kamili na Alice Kariuki.

(Taarifa ya Alice)

UNHCR inasema kanisa hilo Notre Dame de Fatima ni miongoni mwa maeneo ya ibada yaliyoko mji mkuu Bangui, yanayotumika kuhifadhi wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na wakati wa tukio lilikuwa na wakimbizi Elfu Tisa, ikiwemo zaidi ya Elfu waliohamishiwa hapo wiki iliyopita.

Shirika hilo limelaani vikali shambulio hilo dhidi ya wakimbizi wa ndani wakati huu ambapo linaeleza kuwa hali usalama Bangui inazidi kuzorota tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kwani shambulio la juzi ni baya zaidi kutokea tangu kikundi cha Seleka kilipoondoka madarakani mwezi Januari mwaka huu.

Fatoumata Lejeune-Kaba, msemaji wa UNHCR, Geneva amesema kwa sasa kanisa lililoshambuliwa ni tupu..

(Sauti ya Fatoumata)

Waliokimbia kutoka kanisa la Notre Dame de Fatima wamekwenda viungani au maeneo ya kusini mwa Bangui yenye vituo 10 vya wakimbizi wa ndani au eneo jirani la Bimbo. Wengi wamekimbia bila pesa, chakula hata mkeka wa kuweza kujilaza. Wengine wana majeraha ya risasi na wanahitaji huduma ya dharura.”

UNHCR imetaka pande zote kwenye mzozo kulinda raia wasio na hatia na kuzingatia wajibu wao kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu, likisema kuwa hadi sasa makanisa, misikiti na makazi ya watawa ni makazi salama kwa wakimbizi.

Mjini Bangui pekee, kati ya vituo 43 vya wakimbizi wa ndani, 32 ni taasisi za kidini.