Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Denmark yatoa Msaada kwa Shirika la UNICEF nchini Paskistan

Nembo ya UNICEF

Denmark yatoa Msaada kwa Shirika la UNICEF nchini Paskistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchiniPakistan, imepokea masaada kutokaDenmarkya Dola Milioni 11 kufadhili mpango wa miaka mitano kuanzia mwaka wa 2013-2017.

Mpango huo wa kuongeza idadi ya wasichana kupata elimu unatekelezwa  kwenye maeneo ya kikabila yanayosimamiwa na serikali – FATA mkoani Khyber Pakhtunkhwa.

Waziri wa Elimu  wa Pakistan, Mohamed Atif ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwa hafla hiyo, amesema kuwa msaada huo utachangia pakubwa hali ya kuleta usawa ya elimu kwa wasichana ambayo imepewa kipaumbele; kwani hivi sasa kuna tofauti ya asilimia 30 ya wasichana wanaoandikishwa shuleni, ukilinganishwa na ile  ya wavulana ambao ni asiliamia 70.

iendelea kusema kuwa elimu ndiyo itakayozalisha mabadiliko ya kijamii na pia ni suluhu ya shida nyingi zinazokumba nchi kwa jumla.

Waziri huyo alitoa hakikisho kuwa serikali itatekeleza jukumu la kuongeza uandikishaji ya wasichana ili kujiunga na shule, mafunzo  ya ualimu , na pia tecknolojia ya mawasiliano.

Msaada huo ulikabidhiwa na Balozi waDenmarknchini Paskistan -Jesper Moller Sorenzen.