Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani shambulio dhidi ya Makumbusho ya Kiyahudi

UN Photo/Evan Schneider
Baraza la Usalama @

Baraza la Usalama lalaani shambulio dhidi ya Makumbusho ya Kiyahudi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio lililotokea jumamosi, tarehe 24, Mei, katika Jumba la makumbusho ya Kiyahudi, mjini Brussels, Ubelgiji.

Watu watatu, waisraeli wawili na mfaransa mmoja, wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mtu moja, ambaye ametuhumiwa kutekeleza ugaidi huo kwa msingi wa chuki dhidi ya wayahudi.

Wanachama wa Baraza la Usalama wamepeleka rambirambi zao kwa familia ya wahanga pamoja na serikali za Ubelgiji, Israel na Ufaransa.

Kauli ya Baraza la Usalama imelaani aina zote za ubaguzi, na chuki, hasa dhidi ya taasisi ambayo ilikuwa inajitahidi kujenga uvumilivu na upendo.

Wanachama wameongeza kwamba ugaidi ni uhalifu usiokubalika, wakisisitiza umuhimu wa kupeleka watekelezaji, waandaaji na wafadhili wa uhalifu huo mbele ya sheria, na kukumbusha nchi wanachama kuwa ugaidi unahukumiwa chini ya sheria za kimataifa, na vita dhidi ya ugaidi pia vinafaa kuheshimu sheria hizo za kimataifa, na haki za binadamu.