Ban alaani shambulio huko Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati:

29 Mei 2014

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani mashambulio ya hivi karibuni huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwemo shambulio la jana kwenye kanisa la Notre Dame de Fatima kwenye mji mkuu Bangui lililosababisha vifo vya watu kadhada akiwemo padri.

Ban amekaririwa na taarifa ya msemaji wake akisihi serikali ya mpito nchini humo kufanya kila iwezalo kuzuia ghasia zaidi kwenye mji huo na kwingineko nchini kote na kuweka hatua madhubuti ili wanaotekeleza wachukuliwe hatua.

Ametoa wito kwa vikosi vya kimataifa vilivyoko nchini humo hivi sasa kuchukua hatua kuunga mkono juhudi za mamlaka hizo za mpito.

Shambulio la jana limekuja siku chache baada ya lile lililotangulia ambapo vijana watatu wa kiislamu waliuawa kikatili na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Anti –Balaka walipokuwa wakielekea kwenye mechi ya soka yenye lengo la kuleta maridhiano baina ya makabila mbali mbali.

Tayari Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinishwa kupelekwa kwa walinda amani kupitia ujumbe mpya wa MINUSCA utakaoanza kazi Septemba 15 mwaka huu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter