Kongamano la IAEA la kukabiliana na utapiamlo wa kadri lamalizika

29 Mei 2014

Kongamano la siku nne ambalo limekuwa likijikita kwa suala la utapiamlo wa kadri miongoni mwa watoto, likilenga kutambua ni wapi kunahitajika utafiti zaidi ili kuzuia vyema tatizo hilo na tiba yake, limemalizika leo mjini Vienna, Austria, kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA. Joshua Mmali na taarifa kamili

Kongamano hilo la IAEA limeangazia ubunifu wa mikakati ya viwango wastani vya kupima chembechembe za mwili kutumia mbinu za isotopu, ambazo zitasaidia kuongeza nguvu kwa mbinu nyingine zinazotumiwa kufuatilia juhudi za kimataifa za kuboresha lishe ya watoto. Mmoja aliyeshiriki kongamano hilo ni Helen Semu, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu katika Wizara ya Afya nchini Tanzania. Nimemuuliza utapia mlo wa kadri ndio upi hasa

(sauti ya HELEN)

Nimemuuliza pia ni vipi sayansi ya nguvu za atomiki inaweza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo

(sauti ya Helen)

Utapiamlo ni mojawapo ya matatizo sugu zaidi ya kiafya yanayozikabili nchi maskini, na huchangia katika thuluthi moja ya vifo vyote vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter