Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamaduni potofu zisiwe kisingizio cha kukiuka haki za binadamu Morocco: Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay picha ya UM/UNifeed

Tamaduni potofu zisiwe kisingizio cha kukiuka haki za binadamu Morocco: Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ambaye yuko ziarani nchini Morocco, amesema kuwa tamaduni potofu zisitumiwe kama kisingizio cha kukiuka haki za binadamu nchini humo, na wala zisipewe umuhimu zaidi kuliko sheria ya kimataifa na katiba ya Morocco yenyewe?

Pillay amesema ingawa Morocco imepiga hatua katika kuboresha ulinzi wa haki za binadamu tangu ziara ya kamishna mkuu wa haki za binadamu miaka 13 iliyopita, bado kuna vitu vinavyopaswa kufanywa ili kuweka utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu katika taasisi zote za kitaifa Morocco na Sahara Magharibi.

Bi Pillay pia ametoa wito kwa mamlaka za Morocco zianze kutekeleza haraka mpango wa demokraisia na haki za binadamu, ambao ulibuniwa zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Wakati wa ziara yake hiyo ya kuongeza ushirikiano kati ya ofisi yake na serikali ya Morocco kuhusu hali ya haki za binadamu, Bi Pillay amekutana na mfalme wa Morocco, Mohamed VI na viongozi wengine wa ngazi ya juu.