Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapiamlo unaathiri nusu ya watoto wanaokimbia vita CAR

Watoto wanaougua utapiamlo wanapewa chakula maalum hospitali ya Batouri, Cameroun, @UNHCR

Utapiamlo unaathiri nusu ya watoto wanaokimbia vita CAR

Mzozo unaoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati umesababisha zaidi ya watu 85,000 kukimbia nchi hiyo na kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Cameroun, ambapo wengi wao wanapokelewa kwenye kambi za wakimbizi zilizopo mpakani. Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, nusu ya watoto wanaofika kambini wameugua utapiamlo, Adrian Edwards, msemaji wa UNHCR, amewaambia waandishi wa habari kwamba zaidi ya watoto 30 wamefariki dunia kambini kutokana na utapiamlo, mwezi Mei. Katika makala hii, tunapelekwa kwenye kambi ya Gbiti, Cameroun, na Priscilla Lecomte.