Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kutokomeza tabia ya kujisaidia hadharani yazinduliwa UM

Makao Makuu ya UM (picha ya UM)

Kampeni ya kutokomeza tabia ya kujisaidia hadharani yazinduliwa UM

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumezinduliwa kampeni inayonuia kulinda maisha na kukabiliana na umaskini. Taarifa zaidi na Alice Karuki:

(Taarifa ya Alice)

Harakati za kutokomeza tabia za kujisaidia hadharani leo zimeanza upya katika Umoja wa Mataifa kwa kutaka suala hilo lisikaliwe kimya bali lijadiliwe kwani linaleta umaskini, magonjwa kwa watoto na jamii nzima. Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akizindua kampeni hiyo amesema watu Bilioni Mbili na Nusu hawana vyoo duniani.

Amesema kila dakika moja na nusu mtoto mmoja anafariki dunia kutokana na madhara yatokanayo na tabia ya kujisaidia hadharani, jambo ambalo amesema ni aibu kubwa. Eliasson akataka washiriki watulie kwa dakika moja na ndipo akasema..

(Sauti ya Eliasson)

Juhudi hii ya leo ni katika kuchagiza malengo ya maendeleo ya milenia mwakani. Ni mwaka mmoja na miezi saba kabla ya ukomo lakini huduma za kujisafi bado kuna pengo, ni lazima tuchukue hatua sasa. Ningependa kuwakumbusha kuwa dakika moja ya ukimya ya leo si ya upuuzi au kutia aibu, bali mtafakari kwamba iwapo tutashuhudia ukomo wa watu