Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takataka za kielektroniki zakuwa shida kubwa Kenya

@UNEP

Takataka za kielektroniki zakuwa shida kubwa Kenya

Nchini Kenya, tani elfu 17 za takataka za kielektroniki, sawa na simu za mkononi milioni 130, zinatupwa kila mwaka. Changamoto hii imezungumziwa leo katika kongamano lililoandaliwa na shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Taarifa Zaidi na Priscilla Lecomte.

Takataka za kielektroniki ndio sehemu kubwa zaidi ya takataka zote zinazotupwaKenya, na idadi yake inaendelea kuongezeka kutokana na kupungua kwa bei za vifaa vya kielektroniki. Lengo la mkutano wa leo lilikuwa ni kubaini suluhu za kudumu kushughulikia takataka hizo, kwa faida za mazingira na za uchumi.

UNEP imesisitiza kwamba shughuli hiyo ni jukumu la wote. Takataka za kielektroniki ni mchanganyiko wa vifaa vya plastiki na kemikali, ambao ni hatari kubwa kwa mazingira na afya ya binadamu, kwani zimo vipande nururishi, metali nzitokamazebaki au risasi, ambazo zinachafua ardhi na hewa.

UNEP imefanya utafiti katika maeneo ya Dandora, kilomita nane tu kutokaNairobi, ambapo kunatupwa tani elfu 2 za taka kila siku, na imegundulika kwamba nusu ya watoto wanaosoma shuleni pale wameathirika na magonjwa ya mapafu.

Serikali ya Kenyaimeanza kuandaa mkakati endelevu wa kushughulikia, kusafirisha, kutunza na kuhuisha takataka hizo. Dr Faridah Were, mwanatafiti kutoka chuo cha utafiti wa KIRDI, Kenya, ambacho kilishiriki katika kuandaa kongamano hilo, amesema kwamba uhuishaji wa takataka hizo pia ni fursa kubwa ya biashara.