Msafara wa OPCW Syria washambuliwa; hakuna majeruhi

27 Mei 2014

Msafara ya wakaguzi wa jopo la pamoja la Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya kemikali, OPCW umeshambuliwa asubuhi ya leo ulipokuwa ukielekea eneo linalodaiwa kuwepo kwa shambulio la gesi aina ya Klorini.

Imeripotiwa kuwa wote katika mfasara huo wako salama na kwa sasa wamerejea kituoni mwao.

Mkurugenzi Mkuu wa OPCW Ahmet Uzumcu ametoa sikitiko lake na kulaani vikali shambulizi hilo.

Halikadhalika amewahimiza wahusika wa kitendo hicho waache tabia hiyo na badala yake washirikiane na jopo hilo la pamoja la OPCW na umoja wa mataifa.

Aliendelea kusema wakaguzi hao wako Syria ili kubainisha ukweli wa mambo kuhusiana na madai ya kuwepo kwa matumizi ya gesi ya Klorini, hivyo basi usalama wao ni muhimu ili wafanye kazi yao.

Amesema wanataka pande zote za mgogoro nchini Syria ziwapatie usalama na uhuru wa kufikia eneo husika ili watekeleze jukumu lao ipasavyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter