Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani huko Darfur, Sudan wazugumzia fursa zilizopo za amani

Walinda amani walioko Darfur wakiwa katika moja ya doria zao. (Picha:Albert González Farran, UNAMID)

Walinda amani huko Darfur, Sudan wazugumzia fursa zilizopo za amani

Wakati Umoja wa Mataifa utaadhimisha siku ya walinda amani duniani tarehe 29 mwezi huu, mmoja wa walinda amani huko Darfur, nchini Sudan amesema kuna viashiria vilivyojitokeza vyenye dalili za kuleta amani ya kudumu.

Luteni Kanali Furahisha Ntahena wa kitengo cha habari cha ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID amesema hayo alipozungumza na Idhaa katika mahojiano maalum.

(Sauti ya Lt. Kanali Ntahena)

Hata hivyo ametaja changamoto kuwa ni pamoja na..

(Sauti ya Lt. Kanali Ntahena)

Mahojiano kamili na Luteni Kanali Ntahena ambaye anatoka Tanzania yatapatikana kwenye ukurasa wetu.