Ushuru wa tumbaku uongezwe ili kudhibiti wavutaji sigara na tumbaku: WHO
Katika kuelekea siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani tarehe 31 mwezi huu, Shirika la afya duniani WHO limetaka nchi duniani kuongeza ushuru wa tumbaku kwa asilimia 50 ili kupunguza matumizi ya bidhaa zitokanazo na zao hilo.
WHO inasema hatua hiyo ni muhimu kwani katika kila sekunde Sita mtu mmoja anafariki dunia kutokana na tumbaku na zaidi ya hilo tumbaku huleta hasara siyo tu kwa familia bali pia kampuni, serikali na watumiaji wake kwa kuwa husababisha magonjwa kama saratani.
Aidha linasema wanaofariki dunia ni nguvukazi inayotegemewa kwa hiyo ni vyema kodi ikaongezwa kama anavyoelezea Dokta Ayda Yurekli, mratibu kutoka idara ya udhibiti magonjwa , FAO.
(Sauti ya Ayda)
Takwimu zinaonyesha kuwa ongezeko la kodi kwa asilimia 50 litapunguza wavuta sigara na tumbaku Milioni 49 duniani ndani ya miaka mitatu na hivyo kuokoa uhai wa watu Milioni 11
.