Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la wanawake lajihami kukabiliana na changamoto India

Wanawake wa kundi la ujasiri (Picha ya UM/UNIFEED)

Kundi la wanawake lajihami kukabiliana na changamoto India

Wakati uchaguzi ukiwa umemealizika wiki chache zilizopita nchini India na huku idadi ya wanawake waliojitokeza kupiga kura ikiwa kubwa lakini nchi hii inasalia kuwa nchi hatari zaidi kwa wanawake. Ripoti ya Umoja wa Mataifa mwezi huu inasema kwamba idadi ya wanawake walio na nafasi katika ofisi serikalini imepungua. Pia ikiwa na changamoto zikiwemo ndoa za utotoni laikini kuna nuru gizani kufuatia kuanzishwa kwa kikundi cha wanawake ili kukabiliana na changamoto hizi ni Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.