Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utajiri wa bioanuai ya msitu wa hifadhi ya Jozani Zanzibar

kima punju msitu wa Jozani, Zanzibar (Picha ya Idhaa ya Kiswahili/Priscilla Lecomte

Utajiri wa bioanuai ya msitu wa hifadhi ya Jozani Zanzibar

Wakati ulimwengu umeadhimisha siku ya kimataifa ya bioanuai, tarehe 22, Mei, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, linatarajia kupandisha hadhi msitu wa hifadhi ya Jozani,Zanzibarili uwe hifadhi hai ya kimaumbile ya kimataifa kutokana na utajiri wa bioanuai yake hususan kupatikana kwa kima punju au Red Colobus Monkey katika sehemu hii ya pekee ulimwenguni. Lakini msitu wenyewe ukoje? Kulikoni kwa kina, Basi anayetupeleka msitu wa hifadhi ya Jozani ni Priscilla Lecomte