Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yapongeza Korea Kusini kwa juhudi za Kuonda njaa.

Picha ya WFP/Marco Frattini

WFP yapongeza Korea Kusini kwa juhudi za Kuonda njaa.

Mkuu wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin leo amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Korea Kusini kwa kuzindua juhudi za kumaliza njaa duniani kwenye mji mkuuSeoul.

 Akizungumza katika uzinduzi huo Bi Cousin amesema Korea Kusini ni kielelezo cha uwezo wa kuondoa njaa zama hizi kwani awali ilitegemea zaidi msaada wa chakula lakini sasa imeweza kuwa moja wa nchi zinazotoa ufadhili duniani.

Wakati wa ziara yake, Bi Cousin pamoja na waziri wa nchi za kigeni wa Korea Kusini, waliweka saini makubaliano wa mwanzo mpya wa ushrikiano kati ya pande mbili hizo.

Halikadhalika alikutana na viongozi za ngazi za juu serikalini na kuwashukuru kwa misaada za aina mbali mbali aayotolewa na Korea Kusini kwa kuwaeleza kuwa inawezesha kutekeleza mipango na kujenga jamii zenye uhakika wa chakula duniani.