Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni Siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula duniani

UN Photo/Fred Noy
@

Leo ni Siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula duniani

Leo ni siku ya kutokomeza Fistula duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema  ni jambo la kusikitisha kwamba licha ya mafanikio katika mbinu za kisasa za kutoa huduma ya afya lakini takriban wanawake 800 wanafariki dunia kutokana na maradhi yatokanayo na uja uzito kila siku na kwa kila mwanamke anayefariki takriban wanawake 20 wanajeruhiwa au kupata majeraha ya maisha kama vile fistula

Ban amesema Siku ya leo ni fursa ya kupigia chepuo janga  hili ili kuchagiza maendeleo yatakoyochangia kumaliza ugonjwa wa Fistula.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni kufuatilia Fistula-kubadilisha maisha kwani  ugonjwa huo unazuilika Dokta Rutasha Dadi, Mwakilishi msaidizi UNFPA nchiniTanzaniaanaelezea Fistula ni nini..

(sauti ya Dkt. Rutasha)

Katika ujumbe wake Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin amesema kwamba ili kukabiliana na Fistula ni muhimu kufahamu idadi kamili ya wanaougua na wanakoishi, kwani mara nyingi ugonjwa huu hupelekea wanawake kujitenga kutoka kwa familia na jamii