Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay alaani mapinduzi ya kijeshi Thailand

Navi Pilly, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu

Pillay alaani mapinduzi ya kijeshi Thailand

Kufuatia mapindunzi ya kijeshi yaliyofanyika Alhamisi tarehe 22 Mei huko Thailand, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amelaani kitendo hicho na kuiombaThailandiheshimu sheria na haki za binadamu nchini humo.

Imeripotiwa kuwa kamati ya kitaifa ya kutunza amani na utulivuThailandau NPOMC iliyopindua serikali yaThailandimeshatangaza sheria mpya zinazositisha haki ya uhuru wa kujieleza na kuandamana na zingine zikianzisha udhibiti wa vyombo vya habari na Intaneti.

Pillay katika taarifa yake ameelezea wasiwasi zake kuona kwamba serikali ya kuchaguliwa imepinduliwa na haki za binadamu zimekuwa hatarini sasa.