Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawekea vikwazo vya silaha na fedha kikundi cha Boko Haram

(Picha:UN/Marie Gandoi)

UM wawekea vikwazo vya silaha na fedha kikundi cha Boko Haram

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imeongeza kikundi cha Boko Haram kwenye orodha ya watu au taasisi zinazopaswa kuwekewa vikwazo vya kifedha na silaha kutokana na vitendo vyake.

Taarifa ya kamati hiyo iliyotolewa Alhamisi imesema uamuzi huo ni kwa mujibu wa aya ya Kwanza ya azimio namba 2083 la Baraza la Usalama la mwaka 2012 na msingi wake ni kwamba Boko Haram kikiwa mshirika wa kikundi cha kigaidi cha Al Qaeda  na Al Qaeda in the Islamic Mangreb, kinashiriki katika kufadhili, kupanga, kuwezesha na kuandaa au kutekeleza vitendo kwa jina, au kwa niaba au kwa kuunga mkono kundi hilo.

Kufuatia hatua hiyo, mtu yeyote au taasisi ambayo itapatia kikundi cha Boko Haram msaada wa kifedha au vifaa, ikiwemo silaha ataunganishwa katika orodha ya Al Qaeda na atakumbwa na vikwazo.

Kamati hiyo ya vikwazo ya baraza la usalama imesisitiza umuhimu wa usimamizi na utekelezaji wa vikwazo hivyo kama njia fanisi ya kudhibiti vitendo vya kigaidi na imetaka nchi wanachama kujitokeza na kuwasilisha majina ya watu au taasisi zinazohusika na ugaidi.

Nyaraka inayotaja sababu za kujumuishwa kwa Boko Haramu kwenye orodha ya vikwazo imesema kikundi hicho chenye makao yake makuu kaskazini-mashariki mwa Nigeria kimehusika na mashambulizi nchini humo na Cameroon.