Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Ban siku ya kimataifa ya baioanuai

Pomboo aruka majini katika visiwa vya Atauro, Timor Leste (Picha ya UM/Martine Perret)

Ujumbe wa Ban siku ya kimataifa ya baioanuai

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa-Ban Ki-moon ameelzea juu ya umuhimu ya bayoanuai kuwa msingi wa maendeleo.

Bwana Ban amenukuliwa akisema; maadhimisho ya mwaka huu ya baioanuai yanafanyika kwa mwaka “wa visiwa vidogo” vinavyoendelea,- dhamira ikiangazia “anuai za visiwa.”

Watu millioni 600 wanaishi kwa visiwa duniani, ama thuluthi moja  ya watu wote duniani. Inabainika kuwa 1 kati ya nchi tatu  za umoja wa mataifa ni kisiwa. Hivi kwamba baioanuai ni muhimusanakwa ajili ya ustawi, maendeleo na huduma za kijamii.

 Alidokeza kuwa nusu ya rasilimali zilizomo kwa visiwa zinapatikana kwa mabahari, na hivi kwamba haya yanawezesha  shughuli za kitalii, na uvuvi ambazo zina kadiriwa kuleta hadi nusu ya mapato ya visiwa hivyo. Mwamba tumbawe pekee inatoa kiasi cha dola Billioni 375 kwa mwaka kutokana na viumbe tafouti vilivyomo, madawa, chakula na hata mafuta yatokanayo na baioanuai

 Bwana Ban amesihi nchi zote zichukuwe lengo la itifaki ya Nagoya ambayo imeanzisha mbinu za kutumia sayansi za kijenetikikamanjia moja wapo wa kubadili au kupunguza kuzorota zaidi kwa baioanuai. Nchi nyingi duniani zinaendelea kujaribu miundombinu mipya kudhibiti hali hii, kwa kuhifadhi sehemu za pwani na rasilimali zilizomo, haswa visiwani.

Hivi basi, himizo lake kwasiku hii muhimu ni watu kushikamana na kulinda sehemu za mazingira kwa manufaa ya wakaazi wa visiwa na watu wote ulimwenguni.