Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupingwa kwa azimio dhidi ya Syria kwamsikitisha Ban

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon. (Picha:UN/Maktaba)

Kupingwa kwa azimio dhidi ya Syria kwamsikitisha Ban

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Baada ya Baraza la Usalama kushindwa kupitisha azimio la kuwezesha Syria kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kwa mara nyingine tena uhalali wa chombo hicho chenye jukumu la kulinda amani na usalama unatia mashaka.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric amesema Katibu Mkuu amekatishwa tamaa kwa vile Baraza hilo limeshindwa kuwa na sauti moja hasa kwenye jambo muhimu kama hilo..

(Sauti ya Dujarric)

“Iwapo wajumbe wa baraza wanaendelea kushindwa kuafikiana kwenye hatua za kuwezesha uwajibikaji katika uhalifu unaoendelea, uhalali wa chombo hiki na taasisi nzima utaendelea kukumbwa na matatizo, bila kusahau machungu ya wananchi wa Syria na utulivu wa eneo hilo.”

Ban amesema ataendelea kushirikiana na wajumbe wa baraza ili waweke kando tofauti zao na hatimaye wawe na mtazamo mmoja wa kumaliza machungu yanayowakabili wananchi wa Syria.

Katika upigaji kura wa azimio hilo nchi 13 ziliunga mkono huku Urusi yenye kura turufu ikipinga ilhali China yenye kura turufu pia haikuonyesha msimamo wowote.