Ban alaani mashambulizi Nigeria

22 Mei 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani vikali mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya raia nchini Nigeria, ambayo yamesababisha vifo kwa mamia na kujeruhi wengine, akiongeza kuwa hakuna kitu kinachoweza kuhalalisha mashambulizi hayo.

Ban ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za waathirika na kuelezea mshikamano wake na watu na serikali ya Nigeria, huku akiwatakia afueni ya haraka majeruhi wa mashambulizi hayo.

Halikadhalika Ban kupitia kwa msemaji wake amesema anafuatilia kwa karibu hali nchini Nigeria. Kwanzia Mei 12 hadi 15, alituma mwakilishi mkuu wake Nigeria, Bwana Said Djinnit Abuja kujadiliana na serikali kuhusu vile Umoja wa Mataifa unaweza kuchangia katika juhudi za kuachiwa huru kwa takriban wasichana 200 waliotekwa nyara na Boko Haram, na vile vile juhudi za kushughulikia suala la mahitaji ya kibinadamu na hatma ya ukiukwaji wa haki za binadamu .Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria wanatayaraisha mifuko ya baadhi ya mahitaji ya wasichana hao na familia zilizoathirika pamoja na jamii.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter