Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu lakutana kujadili ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Dunia

Mkutano wa Baraza Kuu (Picha ya UM/Evan Schneider)

Baraza kuu lakutana kujadili ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Dunia

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadili jinsi ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Dunia, na ule baina ya nchi za Kaskazini na za Kusini unaweza kuchangia katika kutekeleza ajenda ya maendeleo baada ya 2015. taarifa kamili na Joshua Mmali

(TAARIFA YA JOSHUA)

Mkutano huo wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu umeangazia mchango wa ushirikiano baina ya nchi za Kusini mwa Dunia, ule wa pembe tatu za dunia na ule baina ya nchi za Kaskazini na Kusini, pamoja na teknolojia ya habari na mawasiliano katika utekelezaji wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Ili kufahamu zaidi kuhusu ushirikiano huo, nimezungumza na Bwana Jong-Jin Kim, Mkurugenzi wa Idara ya uchagizaji rasilmali kwa nchi za Kusini mwa Dunia katika Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, ambaye amezungumza kuhusu kinachotakiwa kufanya katika kuongeza hakikisho la chakula kwa kila mtu duniani

Suluhu linapatikana katika juhudi za pamoja katika kutokomeza njaa na utapiamlo, kuongeza uzalishaji wa kilimo kwa njia endelevu na kuboresha mifumo ya chakula ili iwe jumuishi zaidi, na kupunguza umaskini vijijini. Ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Dunia ni njia inayotambulika sasa kama mwafaka zaidi katika kubadilishana suluhu za maendeleo katika nchi zinazoendelea”