Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa CAR wanastahili kutendeka haki: Babacar Gaye asema

Babacar Gaye akizungumza na waandishi wa habari mjini Bangui leo 22 Mei 2014.(Picha: MINUSCA/Dany Balepe)

Raia wa CAR wanastahili kutendeka haki: Babacar Gaye asema

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Babacar Gaye, amezungumza na waandishi wa habari, akisema ni lazima kuhakikisha raia wanatendewa haki.

Amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake unaaendelea kusisitiza umuhimu wa umoja, uadilifu na uhuru wa nchi ya CAR, ndiyo maana ulianzisha mfumo wa vikwazo vya kimataifa, na ametuma mtaalam maalum kuchunguza hali ya haki za binadamu nchini humo.

Licha ya hali ya usalama kuzorota kwenye maeneo mbalimbali, Gaye ameridhishwa na juhudi zilizofanyika kurejesha hali ya utulivu mjini Bangui.

Sauti ya Gaye

“Nataka kwanza kuwapongeza wale wote, kuanzia ngazi ya juu, serikalini, hadi chini katika jamii, ambao wameonyesha kwamba, hapa Bangui, wakristo na waislamu wanaweza kuishi pamoja kwa utulivu na amani. Ndiyo mikakati hii ya kijamii itarejesha hali ya kawaida nchini humo” 

Amerejelea wito aliotoa kwa niaba ya katibu mkuu:

Sauti ya Gaye

“ Lazima wa- Anti-Balaka waheshimu sheria.  Ina maana, lazima wasalimishe silaha zao na wajitayarishe kurejea makwao kwa wale ambao si wakazi wa Bangui. Narejelea pia wito wangu kwa Wa Ex-Seleka.  Wajitayarishe kuingia kwenye mfumo wa DDR, na waheshimu mamlaka ya serikali.”