Ban akiwa China, ataja dira yake kwa dunia itakiwayo

22 Mei 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza katika Chuo Kikuu cha Fudan huko China aliko ziarani na kutaja mambo manne anayoamini kuwa ni dira katika kukidhi mazingira ya dunia itakiwayo na wakazi wake. Joseph Msami na ripoti kamili.

(Taarifa ya Msami)

Ban akihutubia wanafunzi wa Chuo hicho wengi wao wakiwa vijana, mesema tangu mwaka jana Umoja wa Mataifa unatafiti maoni ya watu kuhusu dunia waitakayo na zaidi ya watu Milinoi Mbili nukta Tano wametoa maoni hususan vijana.

Wengi zaidi, wamesema wanataka elimu bora, ajira zenye hadhi na huduma za afya, ikifuatiwa na uaminifu, utawala bora na serikali sikivu.

Hata hivyo amesema kuna changamoto za msingi kuwa na ajenda jumuishi itakayowezesha dunia kuwa na mwelekeo wa ustawi na amani endelevu hivyo akataja mambo manne ya kuzingatia..

(Sauti ya Ban)

“Utulivu, ndipo tuweze kutatua tafouti zilizomo kwa amani. Huruma – kila moja wenu yuko na hamaki. Ni haki na faida kwa vijana kuwa na hamaki lakini ni muhimu zaidi kuwa na huruma. Ushirikiano unafaa ndipo tuweze kutimiza ahadi zetu na kuhakikisha kila jambo limetimilishwa vilivyo. Ujasiri kwa mara nyingine kwa vijana, mtahitaji ushupavu wa kuweza kuyatazamia na kuyaona matarajiyo yenu na kusitisha hizi shida zote, ziwe za kisiasa au za kijamii. Natarajia mkoa na ujasiri huo. Na mwisho ni mwanafalsafa Confucius.”

Katibu Mkuu amehitimisha ziara yake China na yuko njiani kurejea New York.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter