Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu anapaswa kuzingatia anuwai ya tamaduni: Ashe

Tamaduni kama hizi zinachagiza maelewano baina ya wahusika na jamii. (Picha:UN /Logan Abassi)

Kila mtu anapaswa kuzingatia anuwai ya tamaduni: Ashe

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe amewahimiza watu wote duniani kutilia maanani anuwai za kitamaduni ikiwa ni sehemu ya ujumbe wake wa maadhimisho ya anuwai za kitamaduni duniani.

Katika ujumbe huo amesema ili kubadilishana mawazo na maendeleo, angependa kumpa kila moja changamoto ya kutilia maanani hali za utofauti wa kijamii na kuitumia kama kioo kinachoakisi utajiri wa kiutu unaofanya nchi na jamii zote duniani kunawiri.

Bwana John aliendelea kusema kuwa dunia inapokaribia ukomo wa maendeleo ya milenia mwaka 2015, jamii zinaendelea kubuni miundombinu ya kunyanyua maridhiano yatakayomudu hali zote za kiuchumi na kijamii.

Amesema ukweli ni kwamba maendeleo yanafaa kuzingatia mazingira kwa kutegemea rasilimali za nchi na watu wake huku yakiheshimu utamaduni wao.

Ametaka kila mtu kutumia fursa ya siku hii kwa kuweka mikakati ya kufanya maendeleo yenye mafanikio baada ya mwaka 2015.