Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya utamaduni ni kichocheo cha maendeleo-UNESCO

Mabadiliko ya utamaduni ni kichocheo cha maendeleo-UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya anuwai ya utamaduni, shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limesema hazina ya tamaduni mbali mbali duniani ni fursa ya kuwa na maendeleo na amani endelevu. George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Kulinga na ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo imeratibiwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNDP kumekuwa na ongezeko kubwa la ukuaji wa kile kinachoitwa ubunifu wa kiuchumi.

Ripoti hiyo inasema kuwa biashara ya dunia iliyotokana na ubunifu wa huduma na bidhaa ilizalisha kiasi cha dola za Marekani bilioni 624 katika kipindi cha mwaka 2011.

Biashara hiyo ilijitokeza zaidi katika maeneo ya sanaa ya maonyesho ambayo ilipewa mbinu mpya na hivyo kuvutia watu wengi zaidi.

Ripoti hiyo imepongeza hali hiyo na kusema kuwa imesaidia kwa kiwango kikubwa kutoa ajira na kuongeza kipato kwa familia nyingi.