Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban watu 100 waripotiwa kuuawa Nigeria kwa bomu

Nembo la UM

Takriban watu 100 waripotiwa kuuawa Nigeria kwa bomu

Nchini Nigeria, ofisi ya Umoja wa Mataifa inaripoti kuuawa kwa watu 100 katika mashambulio ya bomu katikati mwa mji wa Jos. Joshua Mmali na taarifa kamili.

Afisa wa habari wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Oluseyi Soremekun, ameiambia Redio ya Umoja wa Mataifa kuwa hali ya taharuki imetanda sasa hivi nchini humo, kwani watu hawajui ni nini kitatokea, kufuatia shambulio hili ambalo limefanyika baada ya kutekwa kwa wasichana wa Chibok.

Kama inavyotarajiwa watu wanashuku Boko Haram, ingawa hakuna aliyekiri kuwajibika na mashambulizi haya. Hali ya usalama kaskazini mashariki, ukizingatia hasa hali ya Chibok, linatatanisha shughuli za Umoja wa Mataifa na wadau wengine watoa huduma za kibinadamu.”

Kundi la Boko Haram limehusika katika mashambulizi kadhaa ya bomu nchini Nigeria, pamoja na vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimelaaniwa vikali na maafisa wa ngazi za juu katika Umoja wa Mataifa.