Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknohama ipewe nafasi katika kutimiza ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015

John Ashe (Picha ya UM)

Teknohama ipewe nafasi katika kutimiza ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeanza mjadala wa siku mbili kuhusu nafasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au TEKNOHAMA katika kutimiza ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Mkutano huo unaangalia jinsi ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za kaskazini na kusini, na pia baina ya nchi za kusini zenyewe.

Raisi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, John Ashe, amesema, ili kutimiza malengo haya, ni lazima kuvumbua mikakati bunifu ili kuhakikisha pesa za kutosha zinawekezwa kwa nchi zinazoendelea kwani TEKNOHAMA na ushirikiano katika nchi za kusini zenyewe itachangia zaidi katika kuleta maendeleo endelevu, akiongeza…

(Sauti ya Ashe)

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, naye amesisitiza bado umuhimu wa misaada ya kimataifa, hasa kwa nchi maskini zaidi, akisema:

(Sauti ya Eliasson)

“ Nawapongeza wale ambao wametimiza ahadi zao za utoaji wa misaada, licha ya kukumbwa na shinikizo la bajeti. Ukiwekeza pesa katika kujenga ulimwengu imara, nchi yako yenyewe itafaidika, ndiyo maana ya utandawazi”