Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atolea wito uchaguzi wa amani na jumuishi Malawi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon: Picha ya UM

Ban atolea wito uchaguzi wa amani na jumuishi Malawi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa wagombea uchaguzi, vyama vya kisiasa na taasisi za kitaifa nchini Malawi kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao wa tarehe 20 Mei ni wa amani na unawajumuisha wote.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu ametoa wito kwa wote kutilia maanani azimio la amani la Lilongwe la tarehe 10 Mei, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unaeoukana na ghasia.

Bwana Ban amesema anaamini kuwa harakati za ufanisi za uchaguzi wa urais, ubunge na mabaraza ya mikoa zitakuwa muhimu katika kuimarisha demokrasia nchini Malawi, na akasifu kazi ya tume ya uchaguzi, washiriki wa kitaifa, na wadau wa kimataifa kwa mchango wao katika harakati hizo za uchaguzi.