Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awa na mazungumzo na Rais wa China

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiwa na Rais wa China Xi Jinping baada ya mazungumzo yao mjin Beijing. (Picha: UN /Mark Garten)

Ban awa na mazungumzo na Rais wa China

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziarani huko China amekuwa na mazungumzo na Rais Xi Jinping ambapo wamejadili masuala ya kadhaa ikiwemo usaidizi kwa umoja wa Mataifa na masuala ya mizozo huko Ukraine na Syria

Wamegusia pia amani na usalama ambapo Ban ametoa shukrani zake kwa jinsi China inavyounga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa za kuendelea amani na usalama, maendeleo endelevu na haki za binadamu.

Halikadhalika Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuzuia mizozo akitambua dhima ya China ya uenyekiti wa mkutano wa mashauriano ya kujengeana imani huko Asia, CICA.

Wawili hao pia wamejadili masuala yanayohusiana na amani na usalama barani Asia ikiwemo rasi ya Korea na usalama majini.