Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 67 wa WHO waanza Geneva

Makao Makuu ya WHO

Mkutano wa 67 wa WHO waanza Geneva

Mkutano wa kila mwaka wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO umeanza leo mjini Geneva huku kukitolewa taarifa zinazoonyesha kuwa shirika hilo ni moja ya mashirika duniani yanayoaminiwa zaidi.

 Taarifa kamili na Grace Kaneiya

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu wanaofikia asilimia 72 wana imani kubwa na shirika hilo ambalo linahudumua kwa kiwango kikubwa katika sekta ya afya.

Kiwango hicho ambacho kimeratibiwa na taasisi ya kimataifa ya ukusanyaji maoni ya Gullup kimeshabiana na kile ilichopata shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF. Ama kuhusu mkutano huo wa Geneva, zaidi ya wajumbe wanatarajiwa kuhudhuria wakiwakilisha nchi zaidi ya 194.

Mkutano huo wa 67 unatazamiwa kudumu kwa siku sita na wajumbe watajadiliana kuhusu mambo mbalimbali ikiwamo pia kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukizwa.