Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknohama isaidie kuchagiza maendeleo endelevu: Ban

Teknohama isaidie kuchagiza maendeleo endelevu: Ban

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEKNOHAMA inapaswa kutumika kuinua uchumi wa dunia, kutoa suluhisho la ukuaji wa uchumi na ustawi wa pamoja.

Ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika siku ya kimataifa ya jamii ya mawasiliano na habari hii leo tarehe 17 Mei akitanabaisha kuwa mtandao wa intaneti wenye kasi zaidi ni chombo cha kuwa na nguzo kuu tatu za maendeleo endelevu ambazo ni ukuaji uchumi, jamii jumuishi na mizania kwenye mazingira.

Mathalani amesema intaneti yenye uwezo wa kuchukua vifurushi vikubwa zaidi vya data vinatumika kufanya mawasiliano hata ya kitabibu na kuweza kufikia hata wagonjwa walio maeneo ya ndani zaidi.

Amesema wakati shirika la kimataifa la mawasiliano ITU linaadhimisha miaka 150 mwakani tangu kuanzishwa kwake ni vyema kushrikiana kuondoa pengo la tofauti za kidijitali na wakati  huo huo kutumia teknolojia kuweka maendeleo endelevu kwa wote