Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM wasikititishwa na kuongezeka watu wanaolazimika kutoweka

Nembo ya UM

Wataalam wa UM wasikititishwa na kuongezeka watu wanaolazimika kutoweka

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na suala la watu kulazimika kutoweka, wamesema wanatiwa wasiwasi na idadi kubwa ya visa vilivyoripotiwa kwao hivi karibuni, na kuzitaka serikali kuchukua hatua haraka za uchunguzi wa kina ili kujua hatma ya watu hawa na walipo.

Wataalam wamefanya tathmini ya zaidi ya visa 100 vipya vilivyoripotiwa vya watu kulazimika kutoweka, na kuchunguza vingine 800 vya awali kutoka kwa serikali na vyanzo vingine vya habari kuhusu watu waliolazimika kutoweka.

Visa 38 kati ya hivi 100 vipya ambavyo vimetendeka katika miezi mitatu iliyopita, vilihusu watu kutoka nchi za Bahrain, Cambodia, China, Jamhuri ya Dominica, Misri, Indonesia, Pakistan, Syria, Thailand, United Arab Emirates na Yemen.

Wamesema idadi kubwa ya watu kulazimika kutoweka inabainisha kuwa suala la watu kulazimika kutoweka sio la zamani, na kwamba ni kitu kinachoendelea kutumiwa katika nchi nyingi, huku wakizikuzikumbusha serikali kuwa hakuna muda unaokubalika kwa vitendo hivi kutendeka, hata utowekaji huo uwe wa muda mfupi vipi.