Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya mbinu shirikishi, wazazi wajitokeza watoto kupata chanjo Gabon

Mafunzo kabla ya utoaji chanjo huongeza uelewa miongoni mwa wazazi. (Picha:WHO)

Baada ya mbinu shirikishi, wazazi wajitokeza watoto kupata chanjo Gabon

newuser

11.9999

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Utoaji wa chanjo kwa watoto na hata watu wazima umeendelea kukumbwa na changamoto katika maeneo mbali mbali duniani. Baadhi ya jamii hukataa chanjo, kwa fikra potofu kuwa chanjo zinalenga kutokomeza vizazi katika nchi husika. Wengine hawakubali kutokana na kutokuelewa mambo muhimu ikiwemo wakati wa kupatiwa chanjo hizo. Shirika la afya duniani, WHO linalazimika kutumia mbinu shirikishi ikiwemo elimu kwa wazazi kabla ya kutoa chanjo na hilo limeleta mabadiliko huko Gabon kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi.