Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadilika kwa mfumo wa familia kumeleta changamoto kwa jamii:

(Picha:UM/B Wolff)

Kubadilika kwa mfumo wa familia kumeleta changamoto kwa jamii:

Leo ikiwa ni siku ya familia duniani, Umoja wa Mataifa unazingatia umuhimu wa familia katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia hususan lile la kutokomeza umaskini. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

Licha ya familia kuonekana kitovu cha maendeleo ya jamii iwapo familia itakuzwa katika mazingira bora, changamoto iliyopo sasa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni kuweka mizania ya muda wa kazi na muda wa kuwepo na familia. 

Raymond Mutura, ambaye ni Mkuu wa Jumuiya ya kimataifa ya maendeleo ya familia, IFFD kwa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya kiingereza,ameieleza idhaa hii kuwa ni jinsi gani mawasiliano kati ya mume na mke yanapaswa kubadilika ndani ya familia kutoka na changamoto hizo….

(Sauti ya Mutura)

Pia, ameoyesha faida za mifumo ya familia za kiafrika ambazo huunganisha watu na  ukoo kwa ujumla, ikisaidia kutokomeza upwekee na umaskini kwa jamii.

(Sauti ya Mutura)

Katika maadhimisho ya siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesisitza umuhimu wa kutunza ngazi ya familia katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia  akisema familia zenye nguvu zinalea wananchi ambao watajali jamii yao, na zinaweza kuimarisha hali ya wakina mama, au usawa wa kijinsia...