Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa asili: lazima haki za wanawake zitendeke

Martha Ntoipo, kutoka Tanzania, katika mahojiano.

Watu wa asili: lazima haki za wanawake zitendeke

Kikao cha kudumu kinachohusu haki za watu wa asili kinaendelea hapa New York wiki hii, na washiriki wamekuwa wakizungumzia masuala mbali mbali ambayo yanayahusu hali ya maisha ya watu wa asili.

Redio ya Umoja wa Mataifa imepata fursa ya kuzungumza na Martha Ntoipo, mwanamke kutoka jamii ya kimasai ambaye anapigania haki za wanawake wa kimasai, na kuelimisha jamii kuhusu hatari za ndoa za utoto pamoja na ukeketaji wa wanawake. Ameanza kwa kutueleza umuhimu wa kutunza mila na tamaduni za asili.