Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa wito juhudi zaidi zilenge afya ya vijana barubaru

Vijana baru baru. (Picha-UNESCO)

WHO yatoa wito juhudi zaidi zilenge afya ya vijana barubaru

Shirika la afya duniani WHO limetoa wito kwa seikali kuwekeza zaidi katika afya ya vijana baruabaru. Hii ni kufuatia ripoti iliotolewa na Shirika hilo yenye mada: "Afya kwa vijana barubaru" amabayo inaonyesha kwamba usongo wa akili ni moja ya sababu ya magonjwa na ulemavu wa wavulana na wasichana walio kati ya umri wa miaka 10 hadi 19. Sababu tatu kuu zinazosababisha vifo miongoni mwa vijana barubaru duniani kote ni majeraha yatokanayo na ajali barabarani, virusi vya HIV na ukimwi na kujiua, imesema ripoti hiyo. Ripoti imebainisha kwamba takriban vijana milioni 1.3 walifariki mwaka 2012.

WHO imetaja mambo yanoyathiri vijana kama matumizi ya bidhaa za tumbaku, pombe na madwa ya kulevya, maambukizi ya virusi vya HIV, majeraha, usongo wa akili, lishe, afya ya uzazi na ukatili. Elizabeth Mason ni afisa wa WHO

  CLIP ELIZABETH:

Juhudi ambazo zinahitajika kwa vijana baru baru ni kwa ajili ya afya yao sasa lakini pia maisha yao baadaye wanapokomaa. Na ripoti hii imebainisha hatua tofauti amabazo nchi inaweza kuchukua ili kuimarisha kukabiliana na mahitaji ya kimwili na kiakili na tunatarajia kwamba italenga vijana hususan walio kati ya umri wa miaka 10 hadi 19.”

Katika utafiti wake WHO ilizungumza na vijana kati ya umri wa miaka 10 hadi 19 duniani na kutoa mwelekezo wa jinsi ya kushughulikia masuala yanayoathiri afya ya kimwili na akili kwa vijana baru baru.