Utawala bora unapaswa kujumuisha jamii nzima wakimwemo watu wa asili

14 Mei 2014

Misingi ya utawala bora ni muhimu katika upatikanaji na uwepo wa huduma mbali mbali kwa jamii jumla na hususan kwa jamii za watu wa asili, hiyo ni moja ya hoja ambayo Yannik Mrinyo kutoka wilaya ya gorongoro, Arusha nchini Tanzania anasema wanawasilisha katika kikao cha kudumu kinachohusu haki za watu wa asili kinachoendelea hapa New York.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa kikao hicho Mrinyo amesema kwamba hoja walizonazo ni kutolea serikali wito kusimamia na kuheshimu misingi ya utawala bora kwa maswala mbali mbali ikiwemo

CLIP Yannik

Licha ya kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa huduma kwa watu wa asili ni nyingi ama Mrinyo anasema kwamba ili kuziba pengo ni lazima watu wa asili washirikishwe katika utawala.

CLIP Yannik

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud