Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yazungumzia uhusiano wa homa ya Dengue Tanzania na uhifadhi wa maji

Mbu aina ya Aedes ndiye anayeambukiza ugonjwa wa homa ya Dengue. (Picha-WHO)

WHO yazungumzia uhusiano wa homa ya Dengue Tanzania na uhifadhi wa maji

NchiniTanzaniahoma ya Dengue imeripotiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu na hadi Jumanne ya tarehe 13 Mei 2014 watu watatu wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo ilihali 400 wameugua. Shirika la afya duniani, WHO nchiniTanzanialinashirikiana na serikali kuhakikisha wanadhibiti ugonjwa huo ambao hauna tiba mahsusi bali mgonjwa hupatiwa matibabu ya dalili zinazojitokeza wakati huu ambapo WHO inasema kumekuwepo na ongezeko la ugonjwa huu katika miongo ya karibuni. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Afisa wa udhibiti na uzuiaji wa magonjwa WHO nchini humo Dkt. Grace Saguti na hapa anaanza kwa kuzungumzia hali ilivyo.