Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brahimu ajiuzulu usuluhishi wa mzozo wa Syria, Ban akubali

Lakhdar Brahimi (Picha:UN /JC McIlwaine)

Brahimu ajiuzulu usuluhishi wa mzozo wa Syria, Ban akubali

Mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa kiarabu kwenye mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi, anajiuzulu wadhifa huo kuanzia mwishon mwa mwezi huu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametangaza kukubali hatua hiyo na ametoa msimamo huo mbele ya waandishi wa habari mjiniNew York, akiwa ameambatana na Bwana Brahimi.

Ban amesema anasikitika kuwa pande husika Syria hususan serikali, zimeshindwa kuchukua fursa ya kumaliza mgogoro huo. 

Kwa takribani miaka miwili, mjumbe wa pamoja Brahimi amesaka kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo bado vinaendelea Syria. Amekumbana na mazingira tatanishi na taifa la Syria, Ukanda wa Mashariki ya Kati na hata jamii ya kimataifa ambayo imegawanyika katika hatua za kupatia suluhu mzozo huo.”

Brahimi akizungumza amesema anasikitika kuwa ameiachaSyriakama ilivyo lakini ni matumaini yake kuwa hatua zitachukuliwa kupataSyriailiyokuwepo zamani. Taarifa zaidi baadaye.