Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasikitishwa na vifo vinavyoongezeka kwenye ajali za boti Mediterenia

Manusura wa ajali ya boti kisiwa cha Lampedusa (Picha ya maktaba/UNHCR)

UNHCR yasikitishwa na vifo vinavyoongezeka kwenye ajali za boti Mediterenia

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema limesikitishwa na kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na ajali za boti kwenye Bahari ya Mediterenia mwaka huu, wakati idadi ya wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi salama wakijitosa kwenye vyombo vibovu, mikononi mwa walanguzi wasio na huruma.

Mwishoni mwa wiki, watu wapatao 17 walifariki dunia pale boti yao ilipozama kwenye bahari ya Mediterenia, yapata kilomita 160 kutoka kisiwa cha Lampedusa, Italia, na kilomita 80 kutoka Tripoli, Libya. Miongoni mwa waliokufa ni wanawake 12, watoto watatu na wanaume wawili. Watu 226 waliokolewa na meli mbili za shehena za bidhaa za biashara, meli ya Kifaransa ikawanusuru 158 wengine, na nyingine kutoka Vanuatu kuwaokoa watu 68.

Ajali hiyo inafuatia ajali kadhaa kwenye pwani ya Libya katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, ambapo watu wapatao 121 wanaaminika wamefariki katika visa vilivyohusisha boti tatu tofauti. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)