Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wakubaliana kusukuma mbele agenda ya mabadiliko ya tabia

Achim Steiner NA Waziri Mkuu wa China Li Keqiang

Viongozi wakubaliana kusukuma mbele agenda ya mabadiliko ya tabia

Makubaliano mapya juu ya mabadiliko ya tabia nchi yamefikiwa nchini Kenya Nairobi yakiwahusisha viongozi wa ngazi za juu akiwamo Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya mpango wa mazingira Achim Steiner Waziri Mkuu wa China Li Keqiang.

Pande hizo zimeafikiana kuendelea kushirikiana kwa ajili ya kuyapa msukumo mapendekezo ya kimataifa yanayohusu mabadiliko ya tabia nchi. Pia pande hizo zimeelezea namna zitakavyoshirikiana kusukuma mbele agenda ya inayohusu ulinzi wa mazingira.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili walijadiliana nafasi ya China kusaidia kufanikisha agenda ya mazingira ikiwemo kuhimiza uchumi unaojali mazingira.

China ni moja ya kati ya nchi chache duniani ambazo hutoa sehemu kubwa ya hewa inayochafua mazingira kutokana na shughuli zake.