Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kukabiliana na malaria pwani:Kenya

Mtoto ndani ya neti

Harakati za kukabiliana na malaria pwani:Kenya

Harakati za kukabiliana na Malaria kote ulimwenguni zimeokoa maisha ya takriban watu 3.3 tangu mwaka 2000, huku vifo kutokana na malaria vikiwa vimepungua kwa asilimia 42 kote ulimwenguni na asilimia 49 barani Afika.

Hii ni kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirika la afya ulimwenguni WHO, wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria duniani yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Aprili.

WHO inasema hatua hizo ni kufuatia kuimarika kwa juhudi za serikali na ufadhili zaidi ambao umepunguza kuibuka kwa wagonjwa kutokana na malaria kwa asilimia 25 ulimwenguni na asilimia 31 barani Afrika.

Licha ya hayo, safari bado ni ndefu kwani Malaria bado inawauwa takriban watu 627 000 kila mwaka wengi wakiwa ni watoto chini ya umri wa miaka mitano Kusini mwa Jangwa la Afrika.

Kila mwaka zaidi ya watu milioni 200 huugua kutokana na malaria lakini visa vingi haviripotiwi wala kuchunguzwa.WHO inasema usugu wa dawa ni moja ya changamoto. Wakati Bara la Afrika likibeba mzigo mzito zaidi wa Malaria, Je Afrika mashariki hali iko je. Basi ungana na Salim Chiro wa radio washirika pwani fm ilioko pwani ya Kenya.