Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNDP yupo Tanzania kuangazia ujangili wa wanyamapori na utawala bora:

Mkuu wa UNDP Bi. Helen Clark. (Picha:UM)

Mkuu wa UNDP yupo Tanzania kuangazia ujangili wa wanyamapori na utawala bora:

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP Bi. Helen Clark ambaye anawasili Tanzania leo, baadaye atafunga rasmi mkutano kuhusu ujangili na uhifadhi wa wanyamapori nchini humo.

Mkutano huo huo wa kwanza wa aina yake ukifanyika kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa, serikali ya Tanzania na Kundi la kimataifa la uhifadhi wanyamapori ICCF umekuja wakati ujangili wa tembo ukileta hofu kubwa barani Afrika na kwingineko ambapo Afrika Mashariki majangili wanatumia mbinu za kisasa zaidi.

Phillip Poinsot, Mratibu Mkazi wa UNDP nchini Tanzania amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa na kuelezea matarajio kutoka mkutano huo.

 (Sauti ya Bw. Poinsot)

 “Hatua za kipaumbele za kutokomeza ujangili wa wanyamapori Tanzania, Pili kutakuwepo pain a hatua za kuzuia usafirsihaji haramu wamaliasili za wanyamapori zilizopatikana kinyume cha sheria, halikadhalika hatua za kushirikisha jamii kwenye uhifadhi. Hilo ni suala la  utawala bora, ambapo ni kuhakikisha jamii kwenye maeneo ya mbuga ambazo mara nyingi  zinaishi kimaskini,  zinanufaika na mapato ya sekta inayopata fedha  kutokana na  wanyamapori.”

Pamoja na kufunga rasmi mkutano  huo na kwenda kutembelea mbuga ya wanyama ya Ruaha kuangalia harakati za Umoja wa MAtaifa na serikali ya Tanzania kuhifadhi Tembo, Bi. Clark atakuwa na mazungumzo na viongozi wa serikali na wa mashirika ya kiraia kuhusu masuala ya utawala wa kidemokrasia.

(Sauti ya Poinsot)

“Kutakuwepo pia na fursa ya Bi. Clark kuzungumzia utawala wa kidemokrasia na kuangalia pia msaada ambao umekuwa ukiolewa na UNDP kwenye eneo hili. Lakini pia kuangalia mbele kwenye mambo muhimu yanayotarajiwa kutokea Tanzania.”

UNDP imekuwa ikitoa usaidizi kwa Tanzania katika kuzuia ujangili kupitia makubaliano ya tarehe 20 Machi mwaka 2014 halikadhalika kwenye utawala bora ambapo kupitia mradi wa uwezeshaji kidemokrasia, DEM inatoa usaidizi kadhaa ikiwemo mafunzo kwa watendaji wa Tume ya Taifa ya uchaguzi, NEC na ile ya Zanziba, ZEC.