Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kutaka watoto Nigeria waachiliwe huru yabisha hodi baraza la haki za binadamu

Kikao cha Baraza la Haki za binadamu, Geneva, Uswisi. (Picha-Maktaba)

Kampeni ya kutaka watoto Nigeria waachiliwe huru yabisha hodi baraza la haki za binadamu

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Sisi kundi la wanawake mabalozi katika ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi tunaelezea masikitiko na kuchukizwa kwetu na kutekwa nyara kwa zaidi ya wanafunzi 200 wa kike kutoka shuleni huko Chibok, kaskazini mwa Nigeria na tunataka waachiliwe huru mara moja.

Ni kauli ya Balozi Yvette Stevens, mwakilishi wa Sierra leone huko Geneva, akisoma tamko lao mbele ya baraza la haki la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, ikiwa ni zaidi ya wiki tatu tangu watoto hao watekwe nyara na kundi la Boko Haram.

Amesema kitendo hicho ni kinyume na mikataba, sheria na maazimio ya kimataifa akitaja ibara namba 3,4 na 5 za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa zinazopinga utumwa, kuuzwa utumwani na hata kufanyiwa ukatili.

Balozi Yvette pamoja na kuunga mkono kauli ya Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inayopinga utumwa amesema..

Sauti ya Balozi Yvette)

“Wasichana wetu lazima waachiwe huru mara moja bila masharti yoyote na warejeshwe kwa familia zao. Wasichana wetu lazima waruhusiwe kumaliza masomo yao, mitihani yao na waishi maisha ya kawaida na jamii zao. Wao na familia zao wanahitaji mshikamano wetu na tunaunganisha sauti zetu na za kwao kwa sauti kubwa tukisema.. Rejesha wasichana wetu!”

 

Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Nigeria kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, akashukuru mshikamano uliojitokeza kuhakikisha wasichana hao huku akituma salamu kwa Boko Haram.

(Sauti ya Naibu Mwakilishi wa Nigeria)

 “Serikali ya shirikisho ya Nigeria ina ujumbe kwao. Tukio la kuwateka nyara watoto wasio na hatia huko Chibok ni  mwisho wa vitendo vyao vya kikatili Licha ya mwonekano wa mwelekeo wa hali ilivyo sasa, Rais Goodluck Jonathan ametuhakikishia kuwa tuko katika mwelekeo wa kuwakamata kabisa Boko Haram ili wafikishwe mbele ya sheria.”

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema atatuma mjumbe wake maalum kwenye nchini Nigeria kusaidia kupatia suluhu changamoto zinazokumba nchi hiyo hususan suala hilo la watoto kutekwa nyara.